Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Ahamia ACT

Katika hali ilyowashtua wengi leo hapa Mbeya ni mwenyekiti wa CHADEMA kukihama chama hicho na kujiunga na chama kipya cha ACT.

Tukio hili limetokea leo eneo la Nanenane jijini Mbeya, ni habari za kweli kabisa nimeshuhudia kwa macho yangu sijahadidhiwa,picha nitaweka baadaye kidogo.

Ni mwenyekiti wa wilaya ya Mbeya vijijini jina lake anaitwa ELIA KIOLILE na alitamka machache juu ya chama chake cha zamani kuwa demokrasia ndani CHADEMA ni finyu na inatamkwa kwa maneno tu na si kwa vitendo.

Pia akizungumzia vikosi vya chama hicho vya redbriged kuwa vinajuhusisha na vitendo vya vitisho na mambo ya hatari kama kupiga watu na akasema hataki kuwa sehemu ya dhambi hizo na ndiyo maana ameamua kujiondoa licha ya nafasi aliyonayo ya uenyekiti wa chama wilaya nafasi ambayo alishinda kwenye uchaguzi wa majuzi kwa kupata asilimia 70% ya kura na kutangazwa mshindi.

Pamoja naye, wamehamia pia mtunza hazina wa wilaya Mbeya vijiji na mjumbe wa serikali ya mtaa kwa ticketi ya CHADEMA kata ya Nsalala mtaa wa Zambia road Mbalizi.



0 comments:

Post a Comment

Previous Newer Post
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya Ahamia ACT